Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi. Mary Makondo amekerwa na baadhi ya watendaji wa umma kutokuwa na uchungu na uharibifu wa mali za Serikali katika maeneo wanayosimamia.
Siku ya elimu ya mlipa kodi ya pango la Ardhi imetajwa kuwa mwarobaini katika utatuzi wa migogoro ra Ardhi hasa migogoro inayohusiana na mipaka ya viwanja pamoja na ile ya upimaji juu ya upimaji
Watendaji wa sekta ya Ardhi katika Halmashauri ya Manyoni mkoani Singida, wametakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano na umoja ili kufanikisha utekelezaji wa majukumu yao kwa urahisi zaidi.
Warasimishaji wanaofanya kazi za upangaji na upimaji makazi holela katika mitaa mbalimbali ya mkoa wa Arusha wameagizwa kufanya kazi hizo kwa kuzingatia weledi na maadili ya taaluma zao ili kazi zao zikidhi vigezo vya upangaji na upimaji vilivyowekwa kwa mujibu wa sheria.
Lengo la Serikali kuruhusu urasimishaji ni kumhakikishia mwananchi usalama wa milki yake, kumfanya anufaike na kipande cha ardhi anachomiliki pamoja na hakika ya upatikanaji wa huduma muhimu za kijamii
Serikali inapotoa miongozo ni lazima isimamiwe na itekelezwe ipasavyo. Unaposhindwa kusimamia mkataba wako katika kutoa huduma unakosa uaminifu. Kufanya kazi kwa kusimamia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa ni kuwekeza kwa yule aliyekupa hiyo kazi na kwa Serikali iliyokuamini na kukupa fursa, alisema Bibi Mary.
© 2021 All Rights Reserved.
Site Map
Staff Mail
Designed and Developed bylbl_ega_nam (e-GA) and Contents Managed by Ministry of Lands, Housing and Human Settlements Development