Habari
TUPANGE MATUMIZI BORA YA ARDHI - DKT MWIGULU
- 02 Mar, 2026
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb.) amewataka wananchi kutumia ardhi kulingana na matumizi yaliyokusudiwa ili kuepukana na migogoro ya ardhi.
Waziri Mkuu amesema hayo mapema leo tarehe 02 Machi 2026 wakati alipokuwa akikagua Jengo la mama na mtoto katika hospitali ya Hydom iliyopo katika Halmashauri ya Mbulu Vijijini.
"Hatuna sababu ya kugombana Kuhusu ardhi, kwa Sababu hata tukipigana ardhi haiongezeki " amesema Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba .
Huu ni mwendelezo wa Ziara ya Kikazi ya Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba ambapo leo anatarajiwa kuhitimisha ziara hiyo Mjini Mbulu kwa kufanya Mkutano wa hadhara na kuwasikiliza wananchi.
Aidha, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Kaspar Kaspar Mmuya ameshiriki ziara hiyo akiambatana na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Ardhi Mkoa wa Manyara akiwemo Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Manyara Wenslaus Mtui.