Kurasa
Historia
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imekabidhiwa majukumu kwa Hati Idhini ya Rais (Presidential Instrument) Na. 47 ya tarehe 19 Desemba, 2025. Wizara inatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia muundo ulioidhinishwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 29 Januari 2022 ya kuratibu na kusimamia utekelezaji wa Sera, Sheria na Mipango mbalimbali ya Serikali katika Sekta ya Ardhi. Vilevile, Wizara ina jukumu la kusimamia shughuli za Usimamizi wa Maendeleo ya Ardhi, Upimaji na Ramani, Maendeleo ya Makazi na Uthamini nchini.
Wizara kimuundo imegawanyika katika maeneo makuu mawili ambayo ni:-
1. Usimamizi na Utekelezaji wa Masuala ya Kisekta
Eneo hili linatekelezwa na Idara ya Usimamizi wa Maendeleo ya Ardhi, Upimaji na Ramani na Idara ya Maendeleo ya Makazi kwa ushirikiano na Taasisi zilizopo chini ya Idara hizo.
2. Uendeshaji, Uratibu na Usimamizi
Eneo hili linatekelezwa na Idara ya Sera na Mipango, Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu, Idara ya Uthamini, Kitengo cha Fedha na Uhasibu, Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani, Kitengo cha Ununuzi na Ugavi, Idara ya Huduma za Sheria, Idara ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Kitengo cha Milki, Kitengo cha Usajili wa Hati, Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya pamoja na Kitengo cha Tathmini na Ufuatiliaji.
Kuendelea kutekeleza majukumu ya msingi katika kuboresha huduma za sekta ya ardhi zinazotolewa kwa wananchi kwa maendeleo ya jamii na uchumi.