Kurasa
MAJUKUMU
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inayo majukumu yafuatayo:
- Kuratibu na kusimamia utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Ardhi na Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Makazi;
- Kusimamia Utawala wa Ardhi;
- Kusimamia upangaji na uendelezaji wa miji na vijiji;
- Kusimamia na kuwezesha upimaji wa ardhi na kutayarisha ramani;
- Kumilikisha ardhi na kuwezesha utoaji wa hati za hakimiliki ya kimila;
- Kusajili hatimiliki za ardhi, miamala na nyaraka za kisheria;
- Kusimamia uthamini wa mali;
- Kuhamasisha na kuwezesha ujenzi wa nyumba bora;
- Kusimamia uendelezaji milki;
- Kusimamia utatuzi wa migogoro ya ardhi;
- Kusimamia utunzaji wa kumbukumbu za ardhi;
- Kusimamia ukusanyaji wa maduhuli yatokanayo na huduma za Sekta ya Ardhi; na
- Kuwezesha uandaaji wa mipango ya matumizi ya ardhi na kufuatilia utekelezaji wake