Kurasa

Idara ya Upimaji na Ramani

Idara ina lengo la Kutoa utaalamu na huduma katika uzalishaji na uoneshaji upya wa taarifa za kijiografia kwa ajili ya chati, ramani na michoro ya mipango. Idara ina sehemu tatu ambazo ni Sehemu ya Upimaji wa Topografia, Hidrografia na Jiodesia; Sehemu ya Upimaji wa Kadasta; na Sehemu ya Huduma za Uchoraji Ramani. Idara inatekeleza majukumu yafuatayo: –

i. Kuandaa, kuratibu na kupitia utekelezaji wa sera, sheria, mikakati, programu na miongozo inayohusiana na shughuli za Upimaji na Uchoraji Ramani;

ii. Kufanya na kusimamia utekelezaji wa upimaji wa topografia, hidrografia, jiodesia na kadasta;

iii. Kuratibu na kusimamia utekelezaji wa upimaji wa anga na anga-nje kwa ajili ya ukusanyaji wa takwimu za kijiografia na hatimaye uzalishaji wa taarifa za kijiografia kwa matumizi mbalimbali;

iv. Kubadilisha takwimu za upimaji/kijiografia kuwa chati, ramani na michoro ya mipango; Kusasisha chati, ramani na michoro ya mipango iliyopo;

v. Kukagua na kufanya upimaji wa mipaka ya Taifa na ya Kimataifa;

vi. Kujenga na kuendeleza miundombinu ya Taifa ya uchoraji ramani; na

vii. Kuunganisha na kuratibu mahusiano kati ya Sera ya Taifa ya Ardhi na sera nyingine zinazohusiana na ardhi katika miradi ya upimaji wa maeneo ya vijijini.