Kurasa

Idara ya Usimamizi na Maendeleo ya Ardhi

Idara ina lengo la Kusimamia umiliki na maendeleo ya ardhi nchini kwa ajili ya uhakika wa umiliki na maendeleo endelevu. Idara ina sehemu mbili ambazo ni Sehemu ya Usimamizi wa Ardhi; na Sehemu ya Ukusanyaji wa Mapato ya Ardhi na Uwekezaji. Majukumu ya Idara ni pamoja na: -

i. Kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu masuala yanayohusu utoaji na upatikanaji wa ardhi; Kuandaa, kuratibu na kupitia utekelezaji wa sera, sheria, mikakati, programu na miongozo inayohusiana na Usimamizi wa Ardhi;

ii. Kutoa mapendekezo kuhusu utoaji, uhuishaji na ubatilishaji wa haki za umiliki wa ardhi kwa maeneo yenye maslahi ya Taifa;

iii. Kuendesha uhamasishaji na uelimishaji wa umma kuhusu Sheria za Ardhi;

iv. Kuratibu masuala yanayotokana na kutangazwa kwa upanuzi wa maeneo ya mijini yanayojumuisha ardhi ya vijiji;

v. Kuwezesha upatikanaji wa ardhi, ubatilishaji na uhamishaji wa umiliki wa ardhi;

vi. Kutoa ushauri kuhusu kutangazwa kwa maeneo hatarishi;

vii. Kusimamia uandaaji wa Hati za Haki ya Umiliki wa Ardhi na nyaraka nyingine za usimamizi wa ardhi;

viii. Kuwezesha minada na zabuni za ardhi yenye thamani ya juu; na

ix. Kusimamia utatuzi wa migogoro ya ardhi kwa njia ya kiutawala