Kurasa

Kitengo cha Ununuzi Serikalini

Majukumu ya Kitengo ni kama ifuatavyo: -

i. Kuandaa Mpango wa Ununuzi wa Mwaka wa Wizara;

ii. Kuishauri Menejimenti ya Wizara kuhusu masuala yanayohusu ununuzi wa bidhaa na huduma, pamoja na usimamizi wa vifaa na usafirishaji;

iii. Kufuatilia uzingatiaji wa taratibu na michakato ya ununuzi kwa mujibu wa Sheria ya Ununuzi wa Umma;

iv. Kununua, kutunza na kusimamia vifaa, mali na huduma ili kukidhi mahitaji ya uendeshaji na ugavi wa Wizara;

v. Kuandaa, kuhifadhi na kusasisha orodha ya mali na vifaa vya Wizara;

vi. Kutoa huduma za sekretarieti kwa Bodi ya Zabuni kwa mujibu wa Sheria ya Ununuzi wa Umma; na

vii. Kuweka viwango vya bidhaa na huduma zitakazonunuliwa na kufuatilia uzingatiaji wake ili kuhakikisha thamani halisi ya fedha (value for money).