Kurasa

Idara ya TEHAMA

Majukumu ya idara ni pamoja na: -

i. Kubuni, kuendeleza na kudumisha miundombinu na mifumo ya Tehama;

ii. Kutoa ushauri wa kitaalamu na msaada wa kiufundi kuhusu Tehama na usimamizi wa taarifa na takwimu;

iii. Kuchambua huduma za kielektroniki na kuwezesha matumizi ya Serikali Mtandao (e-Government) ndani ya Wizara;

iv. Kuratibu masuala ya usimamizi wa taarifa na takwimu katika ofisi zote za Wizara;

v. Kuandaa Mkakati wa Tehama wa Taasisi kwa ujumla na Mpango wa Utekelezaji wake;

vi. Kuandaa Miundombinu ya Kisanifu ya Tehama ikijumuisha Usanifu wa Taasisi (Enterprise Architecture), Programu-tumizi, Mitandao/Teknolojia na Usalama wa TEHAMA;

vii. Kutoa huduma za msaada wa TEHAMA kwa watumiaji wote, kuandaa miongozo ya matumizi ya TEHAMA na kufuatilia utekelezaji wake;

viii. Kubuni na kuratibu mafunzo ya Tehama na kujenga uwezo wa watumishi wa TEHAMA katika ngazi zote; na

ix. Kutambua, kuchambua na kutatua changamoto (troubleshooting) za mifumo ya TEHAMA (programu-tumizi na miundombinu) na kutoa suluhisho stahiki.