Kurasa

Kitengo cha Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya

Majukumu ya kitengo ni pamoja na: -

i. Kutathmini utendaji kazi wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya na kutolea taarifa;

ii. Kuyajengea uwezo Mabaraza ili kuleta ufanisi na tija;

iii. Kutoa miongozo ya Utendaji kazi wa kila siku wa Mabaraza;

iv. Kufuatilia na kufanya tathmini ya Utendaji kazi ili kuhakikisha maadili yanafuatwa;

v. Kumshauri waziri mwenye dhamana juu ya ada zinazotozwa kwa ajili ya huduma zitolewazo na Mabaraza; na

vi. Kuwezesha uteuzi wa madalali wa Mabaraza.