Kurasa
Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
Utawala na Rasilimali Watu ni sehemu muhimu katika usimamizi na utekelezaji wa majukumu ya Wizara. Usimamizi huo unafuata sera, sheria na miongozo ya Utumishi wa Umma. Ili kuimarisha utendaji katika sekta ya ardhi, Wizara imehamisha watumishi wa sekta ya ardhi waliokuwa chini ya mamlaka ya OWM TAMISEMI kuwa chini ya mamlaka ya Wizara; na kuwapanga upya watumishi wa sekta ya ardhi katika Halmashauri mbalimbali nchini kwa uwiano. Majukumu ya Idara ni pamoja na: -
i. Kutafsiri na kusimamia matumizi ya Kanuni za Utumishi wa Umma, Kanuni za Kudumu za Utumishi (Standing Orders) na sheria nyingine za kazi;
ii. Kusimamia utekelezaji wa shughuli za kukuza maadili na tunu, ikiwemo elimu ya kuzuia vitendo vya rushwa;
iii. Kusimamia na kuratibu utekelezaji wa shughuli za uajiri, uteuzi, utambulisho wa ajira, mafunzo na maendeleo ya watumishi, upandishwaji vyeo, nidhamu, uhifadhi wa watumishi, motisha, usimamizi wa utendaji kazi na ustawi wa jumla wa watumishi;
iv. Kuhakikisha usimamizi na matumizi bora, yenye ufanisi na tija ya rasilimali watu;
v. Kuratibu masuala ya Baraza la Wafanyakazi na Vyama vya Wafanyakazi;
vi. Kusimamia uandaaji na utekelezaji wa sera, taratibu na miongozo madhubuti ya uajiri, mafunzo na maendeleo, upangaji na uhamishaji wa watumishi, uhifadhi wa watumishi, upandishwaji vyeo na usimamizi wa utendaji kazi;
vii. Kufanya ukaguzi wa rasilimali watu na kuandaa orodha ya ujuzi uliopo na unaohitajika;
viii. Kutoa huduma za kumbukumbu (registry), uhudumiaji wa ujumbe na usafirishaji wa nyaraka, pamoja na kusimamia kumbukumbu za ofisi;
ix. Kushughulikia masuala ya itifaki;
x. Kuwezesha utoaji wa huduma za ulinzi, usafiri na huduma za matumizi ya jumla;
xi. Kuwezesha matengenezo ya vifaa vya ofisi, majengo na mazingira;
xii. Kuratibu utekelezaji wa shughuli za kukuza maadili na miiko;
xiii. Kuratibu utekelezaji wa masuala jumuishi (diversity); na Kuratibu utekelezaji wa ushiriki wa Sekta Binafsi, uboreshaji wa michakato ya biashara na Mkataba wa Huduma kwa Mteja (Client Service Charter).