Kurasa

Kitengo cha Milki

Majukumu ya Kitengo ni pamoja na: -

i. Kushauri juu ya masuala yanayohusiana na sekta ya milki;

ii. Kuandaa na kutekeleza Sera, Sheria, Kanuni na Miongozo inayohakikisha usimamizi mzuri na uendelezaji wa Sekta ya Milki pamoja na usimamizi wa Wataalamu wa Sekta hiyo;

iii. Kufuatilia na kutathmini shughuli za wadau wa sekta ya Milki wakiwemo wamiliki wa nyumba, wapangaji, waendelezaji milki, mawakala wa Milki na taasisi za fedha;

iv. Kuongeza uelewa wa umma na kutoa elimu kwa wadau wa sekta ya Milki;

v. Kuweka utaratibu wa kuhakikisha uwazi na upatikanaji sawa wa fursa na huduma katika sekta ya milki;

vi. Kuanzisha na kudumisha rejesta ya wadau na miradi yote katika sekta ya Milki;

vii. Kufanya utafiti na kusambaza matokeo ya utafiti yatakayoinufaisha sekta ya Milki na Uchumi kwa ujumla;

viii. Kukusanya, kuchakata, kuhifadhi na kusambaza taarifa za sekta ya Milki;

ix. Kuwezesha upatikanaji wa teknolojia mpya kwa ajili ya maendeleo ya sekta ya Milki Kukuza uwekezaji katika sekta ya Milki;

x. Kuweka taratibu za viwango vya utekelezaji wa shughuli za Sekta ya Milki zinazoshughulikia mchakato wa maendeleo ya sekta ikiwemo upembuzi yakinifu, maandalizi ya kabla ya ujenzi, ujenzi, usimamizi wa mali na rasilimali, masoko, ufadhili na uhamishaji wa umiliki; na

xi. Kudumisha ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa kwa ajili ya maendeleo ya sekta ya Milki.