Kurasa
Kitengo cha Huduma za Kisheria
Majukumu ya Kitengo cha Sheria ni pamoja na: -
i. Kutoa ushauri wa kisheria na msaada wa kitaalamu kwa Idara, Vitengo na taasisi zilizo chini ya Wizara;
ii. Kusimamia na kuendesha mashauri ya madai ya kiraia na mashauri mengine yanayofunguliwa na au dhidi ya Wizara, kwa kushirikiana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali;
iii. Kuandaa na kupitia (kuhakiki) mikataba;
iv. Kuandaa na kuhifadhi rejista ya sheria na kanuni zote zinazosimamiwa na kutekelezwa na Wizara;
v. Kusimamia mapitio ya sheria husika na kupendekeza marekebisho yanayohitajika au uundwaji wa sheria mpya;
vi. Kuandaa Kanuni, Sheria Ndogo (Rules) na Tangazo la Serikali;
vii. Kuarifu na kuifahamisha Wizara kuhusu sheria mpya zilizotungwa au marekebisho ya sheria yanayohusiana na majukumu ya Wizara; na
viii. Kuandaa na kuhifadhi rejista ya mashauri yote yanayofunguliwa na au dhidi ya Wizara katika Mahakama ya Rufaa, Mahakama Kuu na Mabaraza (Tribunals).