Kurasa
Kitengo cha Uhasibu na Fedha
Majukumu ya Kitengo ni pamoja na: -
i. Kuhakikisha kuwa Fedha za umma zinazotengwa kwa ajili ya matumizi ya Kawaida, Maendeleo na Amana zinatumika kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia Fedha za Umma;
ii. Kuhakikisha kuwa malipo ya watumishi wa Wizara na Wadau yanalipwa kwa wakati;
iii. Kuhakikisha kuwa Fedha za maduhuli ya Serikali (mapato) zinakusanywa ili kufikia malengo;
iv. Kuandaa Hesabu na Taarifa za Fedha za Wizara; na
v. Kusimamia na kuratibu hoja za ukaguzi.