Kurasa
Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
Majukumu ya Kitengo ni kama ifuatavyo: -
i. Kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa Mipango ya Mwaka na Mpango Mkakati wa Wizara;
ii. Kuandaa taarifa za mara kwa mara za utekelezaji na utendaji;
iii. Kutoa mchango katika maandalizi ya mipango, programu na shughuli za bajeti pamoja na uanzishaji wa viashiria vya utendaji;
iv. Kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu mchakato wa Ufuatiliaji na Tathmini (M&E);
v. Kufanya tafiti kuhusu athari za mipango, miradi na programu zinazotekelezwa na Wizara;
vi. Kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) katika ukusanyaji wa takwimu, uingizaji/uchakataji wa data, uchambuzi na tafsiri;
vii. Kutoa msaada wa kitaalamu wa takwimu wakati wa maandalizi ya mipango na bajeti;
viii. Kuwa msimamizi na kitovu cha takwimu za Sekta;
ix. Kufanya tafiti za utoaji wa huduma ili kukusanya maoni ya wadau/wateja kuhusu huduma zinazotolewa;
x. Kuratibu mapitio ya utendaji ya nusu mwaka na ya mwaka mzima;
xi. Kuratibu utekelezaji wa mikataba ya utendaji (Performance Contracting); na
xii. Kufuatilia utendaji wa Wakala za Serikali, Mashirika ya Umma na Mashirika ya Kisheria yaliyo chini ya Wizara.