Kurasa

Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani

Majukumu ya Kitengo ni pamoja na: -

i. Kupitia na kutoa taarifa kuhusu udhibiti madhubuti wa stakabadhi, uhifadhi na utumiaji ya rasilimali zote za kifedha za Wizara;

ii. Kupitia na kutoa taarifa kuhusu uzingatiaji wa taratibu za kifedha na kiutendaji zilizoainishwa katika sheria, kanuni na maelekezo yanayosimamia udhibiti wa matumizi ya fedha za Wizara;

iii. Kupitia na kutoa taarifa kuhusu uainishaji na ugawaji sahihi wa mapato na matumizi katika hesabu husika;

iv. Kupitia na kutoa taarifa kuhusu usahihi na uadilifu wa taarifa za kifedha na kiutendaji kwa ajili ya uandaaji wa taarifa sahihi za kifedha na ripoti;

v. Kupitia na kutoa taarifa kuhusu mifumo iliyopo ya kulinda mali za Wizara, pamoja na kuthibitisha uwepo wa mali hizo;

vi. Kupitia na kutoa taarifa kuhusu utekelezaji wa shughuli au programu ili kubaini kama matokeo yanaendana na malengo na madhumuni yaliyoainishwa;

vii. Kupitia na kutoa taarifa kuhusu hatua zinazochukuliwa na Menejimenti katika kutekeleza mapendekezo ya taarifa za ukaguzi wa ndani, na kusaidia Menejimenti katika utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG);

viii. Kupitia na kutoa taarifa kuhusu utoshelevu wa mifumo ya udhibiti iliyowekwa katika mifumo ya kielektroniki inayotumika Wizarani; Kuandaa na kutekeleza Mipango Mkakati ya Ukaguzi; na

ix. Kufanya ukaguzi wa utendaji na tathmini ya miradi ya maendeleo.