Kurasa
Idara ya Uthamini
Idara ina lengo la Kutoa utaalamu na huduma katika uthamini wa mali, utozaji wa kodi za mali na ukadiriaji wa pango la ardhi. Idara ina vitengo viwili ambavyo ni Sehemu ya Uthamini wa Jumla na Sehemu ya Viwango vya Kodi za Ardhi. Idara inatekeleza majukumu yafuatayo: -
i. Kutoa ushauri kwa Serikali kuhusu masuala yote ya uthamini wa mali;
ii. Kufanya mapitio ya viwango vya uthamini vitakavyotumiwa na Wathamini wanaofanya kazi kitaaluma;
iii. Kuandaa na kutoa miongozo na taratibu za uthamini wa jumla na usimamizi wa mashauri ya uthamini;
iv. Kutoa taarifa za jumla za uthamini wa mali kwa umma; Kuandaa na kupitia Mwongozo wa Viwango vya Pango la Ardhi kupitia tathmini za upangaji thamani (rating valuations);
v. Kufanya tathmini na kutoa mapendekezo ya ada ya malipo (premium) itakayolipwa wakati wa utoaji wa Haki ya Umiliki wa Ardhi; na
vi. Kushirikiana na taasisi husika katika kurejesha hasara za kifedha zinazotokana na vitendo visivyo vya kimaadili katika shughuli za uthamini.