Kurasa

Idara ya Maendeleo ya Makazi

Idara ina lengo la Kutoa utaalamu na huduma katika upangaji, kuandaa mipango ya matumizi ya ardhi, nyumba na uendelezaji wa makazi endelevu nchini. Idara inasehemu nne ambazo ni Sehemu ya Upangaji na Usanifu miji; Sehemu ya Urasimishaji wa Makazi; Sehemu ya Udhibiti wa undelezaji miji; na Sehemu ya Uendelezaji wa Makazi. Majukumu ya Idara ni pamoja na: -

i. Kutunga, kusimamia, kutathmini na kufanya mapitio ya Sheria, Kanuni za Mipangomiji, Kanuni za Makazi, mikakati mbalimbali ya utekelezaji wa sheria na miongozo;

ii. Kuidhinisha Mipango ya Jumla ya Matumizi ya Ardhi (General Planning Schemes);

iii. Kuidhinisha Mipangokina ya Matumizi ya Ardhi (Detailed Planning Schemes);

iv. Kupanga na kusimamia Mipango ya Jumla na ya kina katika kuendeleza 8 upya maeneo ya kati ya miji (CBD) na maeneo mengine ya miji yaliyochakaa (Redevelopment Schemes);

v. Usimamizi na udhibiti wa uendelezaji wa miji (Development Control);

vi. Kutambua na kusimamia milki na kuboresha miundombinu katika maeneo yasiyopangwa ya pembezoni mwa miji (Settlement Regularisation);

vii. Kufuatilia, kushauri na kusaidia mapitio ya Mipango Kabambe na Mipangokina; Kusimamia na kufuatilia ongezeko la watu, ukuaji wa miji na vijiji na uwepo wa huduma muhimu za ustawi wa miji;

viii. Kusimamia na kufuatilia uendelezaji wa makazi nchini;

ix. Kusimamia uandaaji wa michoro ya Mipango Kabambe na Mipangokina iwe na ubora unakubalika kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Miongozo iliyopo;

x. Kuidhinisha mipango ya kina na ya jumla ya uendelezaji wa mji na utunzaji wa kumbukumbu zake;

xi. Kubuni mikakati ya ushiriki wa sekta binafsi katika upangaji na uendelezaji endelevu wa makazi na huduma zake muhimu;

xii. Kutoa miongozo rafiki kwa vyama vinavyoshiriki katika ubunifu, ujenzi, uendelezaji na usimamizi wa nyumba za gharama nafuu;

xiii. Kusimamia na kufanya utafiti wa uendelezaji wa makazi ya gharama nafuu;

xiv. Kusimamia na kuendeleza watumishi wa sekta ya mipangomiji na nyumba.