Kurasa
Kitengo cha Usajili wa Hati
Majukumu ya Kitengo ni pamoja na: -
i. Kusajili hati na miamala mingine (usajili wa baadaye) ya ardhi kwa mujibu wa Sheria ya Usajili wa Ardhi (Sura ya 334);
ii. Kusajili nyaraka za lazima na za hiari kwa mujibu wa Sheria ya Usajili wa Nyaraka (Sura ya 117);
iii. Kusajili chattels/vyombo (vya kuhamishika/kukodishwa kifedha) kama vile samani, magari, ndege, meli, n.k. kwa mujibu wa Sheria ya Uhamisho wa Chattels (Sura ya 210);
iv. Kutoa ripoti rasmi za utafutaji na kuhifadhi nyaraka kwa maombi;
v. Kuwa na dhamana ya kuhifadhi hati zote na miamala iliyosajiliwa;
vi. Kusimamia, kuanzisha na kuendesha ofisi za usajili wa ardhi;
vii. Kusimamia na kuratibu usajili wa nyaraka na miamala ya ardhi nchini kote kupitia Ofisi za Utawala wa Ardhi za Kanda;
viii. Kufuatilia na kutathmini utendaji wa ofisi za Msajili wa Hati katika Kanda;
ix. Kupitia sheria za usajili na kupendekeza hatua stahiki za marekebisho na mapitio;
x. Kuhudhuria mahakamani pale inapoitwa au kuombwa kwa amri ya mahakama kwa kushirikiana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu;
xi. Kusajili rehani (mortgages); na
xii. Kusajili hati za umiliki wa vitengo na miamala kwa mujibu wa Sheria ya Hati za Vitengo ya mwaka 2008.