Kurasa
Idara ya Sera na Mipango
Malengo
Kutoa huduma za utaalamu na ubora katika utungaji wa sera, utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini.
Kazi
Kuratibu bajeti ya wizara
Kuhakikisha ufuatiliaji na tathmini ya ndani na nje ya shughuli na shabaha za Wizara
Kuweka msingi wa kufanya maamuzi sahihi juu ya mwelekeo wa baadaye wa Wizara
Kuhimiza na kuwezesha utoaji wa huduma kwa Sekta Binafsi katika Wizara
Kutayarisha michango ya Mawaziri kwa Hotuba ya Bajeti na Ripoti ya Mwaka ya Uchumi
Kuweka kitaasisi upangaji mkakati na ujuzi wa Bajeti katika Wizara
Kitengo hiki kinaongozwa na Mkurugenzi na kinajumuisha Sehemu tatu kama ifuatavyo:
Sehemu ya Sera
Sehemu ya Mipango
Sehemu ya Ufuatiliaji na Tathmini