Kurasa

Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali za Watu

Malengo

Kutoa utaalamu na huduma za usimamizi wa rasilimali watu na masuala ya utawala kwa Wizara.

Kazi

  1. Kutoa michango ya kimkakati kwa menejimenti kuhusu masuala ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
  2. Kutoa uhusiano kati ya Wizara na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma kuhusu utekelezaji wa Sera ya Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Ajira ya mwaka 1998 na Sheria ya Utumishi wa Umma namba 8 ya mwaka 2002.

Kitengo kinaongozwa na Mkurugenzi na kinajumuisha Sehemu mbili zifuatazo;

  • Sehemu ya Utawala
  • Sehemu ya Usimamizi wa Rasilimali Watu