Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabula ametoa rai kwa wadau wote wa sekta ya Ardhi wanaojihusisha na miradi ya ujenzi wa nyumba za gharama nafuu kushirikiana na kubadilishana mawazo jinsi gani ya kutekeleza miradi yao.
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeendesha warsha ya kuwajengea uwezo wadau wa masuala ya sekta ya ardhi nchini kuhusu mifumo mbalilmbali inavyotumika katika kutoa huduma kwa wananchi.
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi itajumuika na Ulimwengu wote kuadhimisha Siku ya Makazi Duniani, tarehe 02 Oktoba, 2017 – Karimjee Hall, ambapo Wadau mbalimbali wanategemewa kujumuika katika hafla hiyo, itakayoambatana na Maonyesho.