Habari
DKT AKWILAPO ASHIRIKI KIKAO CHA MAWAZIRI WA WIZARA ZA KISEKTA LUSHOTO TANGA
- 16 Feb, 2026
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Leonard Akwilapo leo tarehe 16 Februari 2026 ameshiriki kikao cha Mawaziri wa Wizara za Kisekta kinachojadili changamoto za sekta ya ardhi zilizojitokeza katika ziara ya Waziri Mkuu Mhe. Dkt Mwigulu Nchemba mkoani Tanga.
Kikao hicho ni utekelezaji wa maelekezo ya Waziri Mkuu Mhe. Dkt Mwigulu Nchemba kuwataka mawaziri hao kukutana haraka na kutafuta suluhu za changamoto zilizojitokeza wakati wa ziara yake mkoani Tanga
Kikao hicho kinashirikisha Mawaziri kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Maliasili na Utalii, Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Kilimo, Maji, Uvuvi na Migugo pamoja na Wizara ya Fedha.
Baadhi ya changamoto zilizoibuliwa wakati wa ziara ya Waziri Mkuu ni malalamiko ya wananchi wa kijiji cha Msomera, Handeni Tanga kudai ardhi yao kuchukuliwa pamoja na mgogoro wa mpaka kati ya wilaya ya Kiteto mkoani Manyara na Kilindi mkoa wa Tanga.