Habari

SERIKALI YAKEMEA MAKAMPUNI YA UPIMAJI YANAYOCHELEWESHA HUDUMA KWA WANANCHI

  • 23 Feb, 2026
SERIKALI YAKEMEA MAKAMPUNI YA UPIMAJI YANAYOCHELEWESHA HUDUMA KWA WANANCHI

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Kaspar Mmuya, ameyaonya makampuni ya upimaji ardhi yanayochukua fedha za wananchi bila kutoa huduma akisisitiza umuhimu wa uwajibikaji na utoaji wa huduma kwa wakati kwa mujibu wa sheria na maadili ya kazi.

 

Mhe. Mmuya ametoa kauli hiyo alipokuwa akisikiliza kero ya mwananchi katika Kliniki ya Ardhi inayoendelea katika Ofisi ya Kata ya Igoma wilayani Nyamagana mkoani Mwanza, ambapo ilielezwa kuwa kampuni ya upimaji ilipokea fedha za huduma lakini haikutekeleza majukumu yake kwa wakati.

 

 "Ukipata nafasi katika maisha ya kutenda wema fanya haraka sana kwa ukubwa wake bila kupoteza muda" amesema naibu Waziri Mmuya. 

 

Zoezi la Kliniki ya Ardhi linaendelea katika maeneo mbalimbali nchini likiwa na lengo la kusogeza huduma karibu na wananchi kukwamua hatimiliki za Ardhi, kusikiliza na kutatua kero pamoja na kuimarisha uwajibikaji kwa watoa huduma katika sekta ya ardhi.