Habari

WIZARA YA ARDHI YAZINDUA MFUMO RASMI WA KUWAHUDUMIA WANANCHI “ARDHI APP”

  • 22 Dec, 2023
WIZARA YA ARDHI YAZINDUA MFUMO RASMI WA KUWAHUDUMIA WANANCHI “ARDHI APP”

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imezindua mfumo rasmi wa kuwahudumia wananchi popote walipo kupitia simu ya kiganjani “Ardhi App” wa kuwasilisha malalamiko ama migogoro ya ardhi katika wizara hiyo.

 

Akizindua mfumo huo Desemba 22, 2023 jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wake na Wahariri wa Vyombo vya Habari kupitia Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa amesema, mfumo huo ni rafika na utawarahisishia wananchi kupata huduma wakiwa katika maeneo yao popote walipo.

 

“Mfumo huu wa “Ardhi App” utakuwa msaada mkubwa sana kwa wananchi wetu, utapunguza gharama na muda wa wananchi kupata huduma katika maeneo mbalimbali nchini, badala yake mwananchi atapata huduma za ardhi kiganjani mwake” amesema Waziri Silaa.