Habari

WIZARA YA ARDHI YATWAA MAKOMBE CRDB BANK BUNGE GRAND BONANZA 2026

  • 21 Jun, 2026
WIZARA YA ARDHI YATWAA MAKOMBE CRDB BANK BUNGE GRAND BONANZA 2026

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kupitia Ardhi Sports Club, leo Juni 20, 2026, imeendelea kung'ara katika CRDB Bank Bunge Grand Bonanza 2026 kwa kutwaa makombe mawili katika michezo ya kuvuta kamba na karata, ikionesha umahiri, mshikamano na ushindani wa hali ya juu.

 

Bonanza hilo lilifanyika chini ya kaulimbiu ya "Pamoja AFCON 2027, Tanzania Tupo Tayari", likiwa na lengo la kuhamasisha na kuelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kujiandaa na kuunga mkono jitihada za Tanzania kuelekea mashindano ya AFCON 2027.