Habari
WIZARA YA ARDHI YATAJA VIPAUMBELE KWA MWAKA 2026/27
- 04 Jun, 2026
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Leonard Akwilapo ametaja vipaumbele vya wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa mwaka wa fedha 2026/2027 wakati akiwasilisha Bajeti ya Wizara hiyo Mei 28, 2026.
Mhe. Dkt. Akwilapo amevitaja vipaumbele hivyo kuwa, ni Kuongeza kasi ya upangaji, upimaji, umilikishaji na usajili wa ardhi mijini, vijijini na maeneo ya kimkakati; kuandaa mipango ya matumizi ya ardhi ya vijiji na kuimarisha mifumo ya TEHAMA katika utunzaji wa kumbukumbu, utoaji wa huduma, ukusanyaji wa maduhuli na upatikanaji wa taarifa za ardhi na uthamini.
Vipaumbele vingine ni kuimarisha mifumo ya utatuzi wa migogoro ya ardhi kwenye Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya; kuhakikisha uwepo wa nyumba bora, ukuaji wa sekta ya milki na maendeleo ya makazi kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii; kuimarisha mipaka ya Kimataifa na kuendeleza miji ya mipakani; kuimarisha upatikanaji wa ramani ili kuwezesha uandaaji wa mipango ya kitaifa na matumizi mengine na kuimarisha mifumo ya usimamizi na ufuatiliaji wa utekelezaji wa vipaumbele.