Habari

WIZARA YA ARDHI YAPIGA KAMBI KLINIKI YA ARDHI MIKOA YA MINNE NCHINI

  • 12 Aug, 2025
WIZARA YA ARDHI YAPIGA KAMBI KLINIKI YA ARDHI MIKOA YA MINNE NCHINI

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imepiga kambi kwenye Kliniki ya Ardhi katika mikoa mitano nchini ili kutoa huduma za ardhi kupitia zoezi la uwamuaji wa urasimishaji wa makazi ya wananchi. 

 

Mikoa hiyo ni Dar es salaam, wilaya ya Ilala, Dodoma, Jiji la Dodoma, Mbeya, wilaya ya Mbarali na Shinyanga, Manispaa ya Shinyanga na Wilaya ya Kahama ambapo timu kutoka Ofisi ya Wizara Makao Makuu kutoka Dodoma inashirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi wa eneo husika pamoja na watumishi wa Ofisi ya Kamishna Msaidizi wa mkoa husika wanaendelea kutoa hatimilki za ardhi katika maeneo husika. 

 

Katika mkoa wa Dar es salaam, timu hiyo inashirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi wa Ilala jijini Dar es salaam ambayo imepiga kambi katika Kata ya Kivule kuendesha zoezi la Kliniki ya Ardhi na kutoa Hatimiliki za Ardhi kwa wananchi baada ya kukamilisha zoezi la ukwamuaji wa urasilishaji wa makazi ya wananchi hao.

 

Kliniki hiyo ya siku 14 inafanyika ilianza Agosti 5, 2025 na inatarajiwa kuhitimishwa Agosti 18, 2025 ambapo wananchi wanaendelea kutapata huduma za ardhi ikiwemo Hatimiliki na kutatua migogoro mbalimbali ya ardhi katika maeneo yao.