Habari
WIZARA YA ARDHI YAIDHINISHIWA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 210.2
- 04 Jun, 2026
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania likeidhinisha kiasi cha Shilingi bilioni 210,259,515 kwa ajili ya utekelezaji wa Bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa mwaka wa fedha 2026/2027
Kati ya fedha hizo zilizoidhinishwa na Bunge, shilingi 100,224,553,000 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Shilingi 39,090,003,000 ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyo (OC).
Aidha, Shilingi 110,034,962,000 zitatumika kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo ambapo kati ya fedha hizo Shilingi 44,132,469,000 ni Fedha za Ndani na Shilingi 65,902,493,000 ni Fedha za Nje.
Awali Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Leonard Akwilapo aliliomba Bunge kuidhinisha kiasi hicho cha fedha ili iweze kutekeleza vipaumbele na mpango wa Bajeti Kwa mwaka wa fedha 2026/2027.