Habari

WAZIRI SILAA AUNDA KAMATI KUMALIZA MGOGORO WA ARDHI SAME

  • 29 Jan, 2024
WAZIRI SILAA AUNDA KAMATI KUMALIZA MGOGORO WA ARDHI SAME

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa ameunda kamati maalum kwa ajili ya kukusanya taarifa za kutatua migogoro wa ardhi katika vijiji vya Bangalala, Mwembe na Makanya vilivyopo wilayani Same Mkoani Kilimanjaro.

 

Waziri Silaa amechukua hatua hiyo wakati alipofanya mkutano wa hadhara na wanakijiji hao akiongozana na Mkuu wa wilaya ya Same Bi. Kasilda Mgeni kwa lengo la kutatua migogoro ya umiliki wa maeneo inayovikabili vijiji hivyo vinavyopaka.

 

Kamati hiyo inaundwa na wawakilishi wa wananchi kutoka vijiji hivyo, Kamishna wa Ardhi kutoka Wizarani, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Same pamoja na Wataalamu wa Ardhi.

 

Waziri Silaa amesema anataraji kufanya maamuzi juu ya mgogoro huo mara baada kupokea taarifa kutoka kwa kamati hiyo aliyounda mwenyewe.