Habari
WAZIRI NDEJEMBI ASHIRIKI MKUTANO WA KAWAIDA AU, MAENDELEO YA MIJI
- 22 Dec, 2024
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Deogratius Ndejembi ashiriki kikao cha tano cha kawaida cha kamati maalum ya Umoja wa Afrika kuhusu Huduma za Umma, Serikali za Mitaa na Maendeleo ya Miji.
Kikao hicho kimefanyika jijini Tunis, Tunisia Desemba 18-20, 2024 na kuwahusisha Mawaziri wa kisekta kutoka Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika na kuhudhuriwa pia na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora, Mhe George Simbachawene.