Habari
WANAWAKE ARDHI WASHIRIKI KONGAMANO LA WANAWAKE DODOMA
- 06 Mar, 2025

Ardhi ni rasilimali kuu ya maendeleo kiuchumi, kijamii na ustawi wa watu wote
Wanawake kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wameshiriki Kongamano la Wanawake ambalo limefanyika Machi 3, 2024 jijini Dodoma ikiwa ni shamrashamra za kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo huadhimishwa Machi 8 kila mwaka.
Kongamano hilo limewakutanisha Wanawake kutoka mikoa mitatu ambayo ni Dodoma wenyeji, Singida na Iringa.
Akifungua kongamano hilo, Mgeni rasmi kwenye Kongamano hilo alikuwa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda.
Maadhimisho hayo kitaifa yatafanyika Jjijini Arusha na Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kaulimbiu ya mwaka huu
Adhimisho hayo ni "Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji"