Habari

WANANCHI WACHANGAMKIA FURSA ZA HATI KATIKA KLINIKI YA ARDHI MISENYI

  • 20 Nov, 2025
WANANCHI WACHANGAMKIA FURSA ZA HATI KATIKA KLINIKI YA ARDHI MISENYI

Wananchi wilayani Misenyi mkoani Kagera wamechangamkia fursa ya utolewaji Hati Milki za Ardhi pamoja na huduma nyingine za sekta ya ardhi katika Kliniki ya Ardhi inayoendelea kwenye mji wa Mutukula.

 

Jumla ya Hati Miliki za Ardhi 50 zimetolewa kwa wananchi wa Mutukula wakati katika mji wa Kyaka Hati Miliki za Ardhi 12 zimetolewa hadi kufikia Novemba 19, 2025.

 

Kliniki hiyo ya ardhi iliyoanza Novemba 17, 2025 na kuhitimishwa Novemba 21, 2025 inaendeshwa kwa ushirikiano wa ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kupitia Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Kagera.