Habari

WANANCHI 429 WAGAWIWA HATIMILIKI ZA KIMILA KIJIJI CHA MAYUYA, SENGEREMA

  • 11 Sep, 2026
WANANCHI 429 WAGAWIWA HATIMILIKI ZA KIMILA KIJIJI CHA MAYUYA, SENGEREMA

Serikali imegawa jumla ya Hatimiliki za Kimila 429 kwa wananchi wa Kijiji cha Mayuya, Kata ya Tabaruka katika Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema ikiwa ni juhudi za kuimarisha usalama wa milki za ardhi na kuwapatia wananchi nyaraka rasmi za umiliki.

 

Ugawaji wa hati hizo utaongeza usalama wa umiliki wa ardhi, kupunguza migogoro na kuwawezesha wananchi kutumia ardhi yao kama rasilimali yenye thamani kwa maendeleo ya familia na jamii.

 

Hafla hiyo imehudhuriwa viongozi mbalimbali akiwemo Bwana Ally Salimu kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Mhe. Senyi Ngaga, Afisa Maendeleo ya Ardhi wa Wilaya, Bwana Renatus Nyasebwa pamoja na wataalam kutoka GMS Geotech Consultancy Co. Ltd, kampuni inayotekeleza mradi wa upimaji ardhi na uwezeshaji wa wananchi kupata Hatimiliki za Kimila katika eneo hilo.