Habari

WANANACHI WAMIMINIKA KIVULE KUPOKEA HATIMILKI ZA MAENEO YAO 

  • 12 Aug, 2025
WANANACHI WAMIMINIKA KIVULE KUPOKEA HATIMILKI ZA MAENEO YAO 

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inaendesha zoezi la Kliniki ya Ardhi Mkoa wa Dar es salaam Manispaa ya Ilala Kata ya Kivule na kutoa Hatimiliki kwa wananchi ambao wamekamilisha nyaraka za umiliki baada ukwamuaji wa urasimishaji wa maeneo yao mitaa ya Kivule, Magole A, Kerezange na Bomba mbili.

 

Kliniki hiyo ni utekelezaji wa maelekezo ya Mhe. Deogratius Ndejembi Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliyoyatoa Desema 2024 kuhakikisha maeneo yote ili kukamilisha ukwamuaji wa urasimishaji kwa kuweka mawe ya upimaji (Bicon) katika maeneo yaliyofanyiwa urasimishaji ili wananchi wapewe hati za maeneo yao.

 

Maeneo mengine ambayo zoezi hilo linafanyika ni Magole mtaa wa Mbondole na Kitonga, Kata ya Zingiziwa mtaa wa Lubakaya, Bonyokwa, Kinyerezi, Kanga, Amani, Liwiti, Mogo, Sabasaba, Uwanja wa Ndege, Kitinye, Kiuombo na Kipera Relini.

 

Timu inayofanya kazi hiyo inaongozwa na Mthamini Mkuu kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi. Evelyn Mugasha na watumishi kutoka Ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Dar es salaam na linatarajiwa kuhitimishwa Agosti 18, 2025.