Habari

VIONGOZI WAWATAKA WANANCHI BAGAMOYO KUWASILISHA KERO ZA ARDHI KWA UWAZI

  • 21 Oct, 2026
VIONGOZI WAWATAKA WANANCHI BAGAMOYO KUWASILISHA KERO ZA ARDHI KWA UWAZI

Kamishna wa Ardhi, Nathaniel Nhonge, akizungumza na wananchi katika eneo la Shule ya Msingi Majengo, Bagamoyo, Oktoba 19, 2026, kabla ya kuanza kusikiliza na kushughulikia changamoto zao za ardhi.

 

Katika mazungumzo hayo, Nhonge amesisitiza umuhimu wa kutoa huduma kwa wakati na kuzingatia mahitaji ya wananchi, hususan wazee na watu wenye mahitaji maalumu, ili kuhakikisha wanapata huduma kwa haki na kwa kuzingatia mazingira yao.

 

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Shaibu Ndemanga, amewataka wananchi kuwa wazi wanapowasilisha changamoto zao kwa wataalamu wa ardhi, ikiwemo kueleza muda ambao changamoto hizo zimekuwepo na hatua zilizokwisha kuchukuliwa, ili kurahisisha utambuzi wa matatizo na hatua za kuyatatua.

 

Naye Naibu Kamishna wa Ardhi, Hussein Sadick, akizungumza na wananchi kabla ya kuanza kusikiliza hoja zao, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya wananchi na wataalamu wa ardhi katika kufanikisha zoezi la usikilizaji na utatuzi wa changamoto zinazowakabili.

 

Hii ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, la kushughulikia changamoto za ardhi katika maeneo yanayohitajika kwa uwekezaji kwenye Eneo Maalumu la Kiuchumi la Bagamoyo, mkoani Pwani.