Habari

Ukimdhulumu mtu yeyote katika mchakato wa kupata hati wewe umejitafutia matatizo: Naibu Waziri Kaspar Mmuya

  • 04 Mar, 2026
Ukimdhulumu mtu yeyote katika mchakato wa kupata hati wewe umejitafutia matatizo: Naibu Waziri Kaspar Mmuya

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Kaspar Mmuya amewatahadharisha watu wanaofanya ulaghai kwa wananchi katika mchakato wa kupata hatimiliki za ardhi kwamba sheria itachukua mkondo wake endapo watabainika.

 

Mhe. Mmuya amesema hayo leo tarehe 03 Machi 2026 alipotembelea Ofisi za Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Dodoma ambapo zoezi la kuwahudumia wananchi lijulikanalo kama Samia Ardhi Kliniki inaendelea kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.

 

"Msikubali wananchi hakuna udalali wala mtu kati katika mchakato wa kupata hati" amesema Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Kaspar Mmuya.