Habari

UHAKIKI WA VIWANJA NA UPIMAJI ARDHI IPALA NA MAHOMANYIKA DODOMA WAONGEZA TUMAINI, WANANCHI  WAIPONGEZA SERIKALI KWA HATUA MADHUBUTI

  • 12 May, 2026
UHAKIKI WA VIWANJA NA UPIMAJI ARDHI IPALA NA MAHOMANYIKA DODOMA WAONGEZA TUMAINI, WANANCHI  WAIPONGEZA SERIKALI KWA HATUA MADHUBUTI

Zoezi la uhakiki wa viwanja na upimaji wa ardhi katika kata za Ipala na Mahomanyika linaendelea kwa kasi ya kuridhisha, likiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, pamoja na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Leonard Akwilapo, na tayari limeanza kuleta matumaini mapya kwa wananchi huku mafanikio yake yakionekana kwa vitendo. 

 

Wakizungumza katika maeneo hayo leo tarehe 6 Meli 2026 baadhi ya wananchi Charlse Richard Madea,Peter Msonga na Bi.Sara Zakayo wameeleza furaha na kuridhishwa kwao, wakibainisha kuwa hatua hiyo ni chachu ya maendeleo na suluhisho la kudumu kwa changamoto za migogoro ya ardhi. 

 

Wananchi hao wameishukuru Serikali kwa kuwafikishia huduma hiyo muhimu inayowawezesha kumiliki ardhi zao kisheria na kupanga makazi yao kwa utaratibu bora zaidi. 

 

Aidha, wamepongeza juhudi na weledi wa wataalamu wa ardhi wanaoendelea kusimamia zoezi hilo kwa ufanisi, wakionesha dhamira ya dhati ya kuhakikisha linakamilika kwa wakati na kuleta manufaa makubwa kwa jamii kwa ujumla.