Habari

TANZANIA YASHIRIKI UZINDUZI WA MKUTANO WA SHAFDB NCHINI MOROCCO

  • 10 Jun, 2026
TANZANIA YASHIRIKI UZINDUZI WA MKUTANO WA SHAFDB NCHINI MOROCCO

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, leo imeshiriki katika Uzinduzi rasmi wa Mkutano Mkuu wa 45 wa Mwaka na Kongamano la Benki ya Maendeleo ya Makazi ShafDB unaofanyika jijini Rabat, Morocco tarehe 9 hadi 11 2026.

 

Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo unaongozwa na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Kaspar Mmuya (Mb.) ambapo Tanzania inashiriki kimkakati kwa lengo la kuimarisha diplomasia ya kiuchumi, kuvutia mifumo mipya ya kifedha, na kupata mitaji ya muda mrefu kupitia ShafDB kwa ajili ya kuendeleza miradi mikubwa ya makazi bora na ya gharama nafuu nchini. 

 

Hatua hii inatarajiwa kuleta mageuzi makubwa ya ujenzi wa makazi yanayohimili mabadiliko ya tabianchi na kuongeza fursa za kiuchumi kwa sekta rasmi na isiyo rasmi nchini.

 

Mkutano huo wa siku nne utaongozwa na kauli mbiu isemayo "Mustakabali wa Miji: Kugharamia Maendeleo ya Miji Jumuishi, ya Kijani na Yanayohimili Mabadiliko ya Tabianchi".