Habari
SINGIDA YAANZA KUTOA HATI MILIKI ZA ARDHI KUPITIA MFUMO WA e-ARDHI
- 21 Sep, 2026
Mkoa wa Singida umeanza rasmi kutoa hati Milki za Ardhi kupitia mfumo wa e-Ardhi ambapo sasa wananchi hawatalizimika kufika ofisi za ardhi katika mkoa huo kufuatilia maombi yao ya umiliki wa ardhi kama ilivyokuwa zamani.
Bi. Nzito Enock mkazi wa Kata ya Mandewa amekuwa mwananchi wa kwanza katika mkoa wa Singida kupata hati milki kupitia mfumo huo na kuuelezea kuwa, ni rahisi na unaokoa muda ambapo amebainisha kuwa, yeye mwenyewe ameweza kupata hati yake ndani ya siku moja.
Utoaji wa hati hizo umefanyika leo, Septemba 19, 2026, ukiongozwa na Kamishna wa Ardhi Mkoa wa Singida, Bi. Shamimu Hoza aliyeelezea zoezi hilo kuwa ni mwendelezo wa matumizi ya mfumo wa e-Ardhi.
"Niwahimiza wananchi kufika Ofisi za Ardhi Mkoa wa Singida kupata elimu zaidi kuhusu mfumo huu na namna ya kuutumia". amesema Bi Shamim
Ameongeza kuwa, mfumo wa e-Ardhi unarahisisha upatikanaji hati na kupunguza migogoro ya umiliki ambapo Kupitia mfumo huo hati miliki inapokuwa imetolewa kwa kiwanja, mfumo hauruhusu kutolewa kwa hati nyingine kwa kiwanja hicho hicho.