Habari

SERIKALI IMEANZISHA KLINIKI YA ARDHI KUWAHUDUMIA WANANCHI KWA KARIBU ZAIDI

  • 07 Mar, 2025
SERIKALI IMEANZISHA KLINIKI YA ARDHI KUWAHUDUMIA WANANCHI KWA KARIBU ZAIDI

Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imesogeza Kliniki za Ardhi karibu na wananchi ili wapate huduma kwa urahisi zaidi.

 

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Deogratius Ndejembi anaendelea kusikiliza na kutatua changamoto za ardhi zilizoletwa na wananchi kutoka sehemu mbalimbali za Mkoa wa Arusha katika Kliniki ya Ardhi inayofanyika katika Mtaa wa Soweto jijini Arusha Machi 06, 2025.

 

Mhe. Waziri ameambatana na Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga, Kamishna wa Ardhi Nathaniel Mathew, Mthamini Mkuu wa Serikali Evelyn Mghasha na Watendaji wa Wizara.