Habari

RAIS DKT. SAMIA AMUAPISHA DAVID SILINDE KUWA WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI

  • 27 Nov, 2026
RAIS DKT. SAMIA AMUAPISHA DAVID SILINDE KUWA WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Novemba 27, 2026, amemuapisha rasmi Mhe. David Ernest Silinde kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika hafla ya uapisho iliyofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam.

 

Uapisho huo unaashiria mwanzo wa utekelezaji wa majukumu ya Mhe. Silinde katika kuongoza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ikiwemo kusimamia sekta ya ardhi, kuimarisha usimamizi wa rasilimali za ardhi na kuendelea kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

 

Hafla hiyo imehudhuriwa pia na Viongozi mbalimbali wa serikali na Wizara.