Habari
NDEJEMBI AKUTANA NA VIONGOZI WA JUMUIYA YA WAISLAMU WA AHMADIYYA
- 09 Jan, 2025
![NDEJEMBI AKUTANA NA VIONGOZI WA JUMUIYA YA WAISLAMU WA AHMADIYYA](https://www.lands.go.tz/uploads/news/b839591061a3dcdff2a63fb009687281.jpeg)
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Deogratius Ndejembi amekutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya Tanzania yenye lengo la kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya ardhi nchini.
Kikao hicho kimefanyika Januari 08, 2025 Ofisi za Makao Makuu ya Wizara zilizopo Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.
kikao hicho ni kilihudhuriwa na Balozi wa Tanzania, Umoja wa Mataifa, Mhe. Hoyce Temu, Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Mwanaisha Ulenge na Viongozi wa Jumuiya hiyo wakiongozwa na Amiri na Mbashiri Mkuu wa Jumuiya ya Ahmadiyya Nchini, Sheikh Khawaja Muzaffar Ahmad.