Habari
NDEJEMBI AAGIZA KUFUTWA HATI MILKI YA ARDHI RUVUMA
- 23 Sep, 2024
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Deogratius Ndejembi amemuelekeza Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Ruvuma kuifuta Hati ya Ardhi kwa Bw. Steven Mapunda ambaye alikabidhiwa bila kufuata utaratibu katika Kijiji cha Mwanamango Manispaa ya Songea.
Mhe. Ndejembi ametoa agizo hilo Septemba 22, 2024 baada ya kufika katika kijiji hicho kutatua mgogoro wa ardhu uliodumu kwa muda mrefu.
Mgogoro huo unamuhusisha Bw. Mapunda aliyemilikishwa ekari 45 za mashamba ya wananchi wa Mwanamango bila kuwalipa fidia kama sheria inavyoelekeza.
“Ninamuelekeza Kamishna wa Ardhi wa Mkoa kufuta hati ya Bw. Mapunda kwa sababu wananchi hawakushirikishwa na wala hawakulipwa fidia. Kwa hiyo maamuzi yangu leo ni kwamba hiyo hati iondolewe papimwe tena na wananchi wamilikishwe maeneo yao kwa mujibu wa sheria.