Habari
NAIBU WAZIRI PINDA AKABIDHI HATI 250 ROMBO
- 19 Sep, 2024
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi mhe. Geophrey Pinda amekabidhi jumla ya Hatimiliki za Ardhi 250 kwa wananchi wa Tarakea wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro.
Mhe. Pinda amekabidhi hati hizo leo tarehe 18 Septemba 2024 katika hafla fupi iliyofanyika Soko la Mbomai Wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro ambako Kliniki ya Ardhi inafanyika.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Naibu Waziri wa Ardhi Mhe. Pinda amewataka wananchi waliokabidhiwa hati kuhakikisha wanazihifadhi na kuzitunza kwa umakini pasipo kuifungasha na vitu vigumu (Lamination).
Amesema, hati milki za ardhi walizokabidhiwa wananchi wa Rombo ni nyaraka nyeti na zina faida kubwa ikiwemo kuaminiwa kupata mikopo kutoka taasisi za kifedha nchini.
Kadhalika Mhe. Pinda amemuelekeza Kamshina wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Kilimanjaro Bi. Rehema Jato kuendesha tena zoezi la kliniki ya Ardhi katika Wilaya ya Rombo kwa siku tatu kuanzia Septemba 25 hadi 27 Mwaka huu
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Grophrey Pinda yuko katika ziara ya kikazi mkoni Kilimanjaro ambapo mbali na mambo mengine atasikiliza na kutatua changamoto za ardhi kwa wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro.