Habari
NAIBU WAZIRI MMUYA AONGEZA SIKU NNE KLINIKI YA ARDHI IGOMA, MWANZA
- 18 Feb, 2026
- Awahimiza wataalamu wa kujitoa kuwahudumia wananchi.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Kaspar Mmuya amefika katika zoezi la Kliniki ya Ardhi inayoendelea katika Ofisi ya Kata ya Igoma mkoani Mwanza kujionea zoezi hilo lenye lengo la kuhakikisha kila mwananchi anayemiliki kipande cha ardhi anapatiwa hati.
Ili kuhakikisha lengo la kuwapatia wananchi hati linafikiwa, Naibu Waziri Mmuya kwa niaba ya Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo ameongeza siku nne za kuendelea kutoa huduma na kuhakikisha wananchi wote wanaowasilisha maombi ya kupata hati.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri Mmuya amewaasa wataalamu kuwa wavumilivu na kujitoa kwa moyo wa dhati kuwahudumia watanzania ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan za kufanya kazi kwa kuzingatia utu na kuwapa tabasamu watanzania kupitia Sekta ya Ardhi.