Habari

NAIBU KATIBU MKUU ARIDHISHWA UFYATUAJI WA BIKONI DAR

  • 26 Nov, 2024
NAIBU KATIBU MKUU ARIDHISHWA UFYATUAJI WA BIKONI DAR

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi. Lucy Kabyemera ametembelea na kufanya ukaguzi wa ufyatuaji wa bikoni unaoendelea mkoani Dar es salaam ambapo zaidi ya bikoni 32,000 kati ya 48,000 zimefyatuliwa.

 

Bi Kabyemera ameupongeza Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) pamoja na Mkandarasi wa kazi hiyo kwa kazi wanayoendelea kuifanya kwani bikoni hizo zitaenda kupunguza au kumaliza kabisa migogoro ya mipaka baina ya wananchi.

 

Aidha, Bi Kabyemera amemshukuru na kumpongeza Diwani wa Kata ya Kivule Mhe. Nyansika Getama kwa kutoa ushirikiano wakati kazi hiyo ikiendelea katika eneo lake kwani ulinzi umeimarishwa na hakuna uharibifu wowote uliojitokeza kwenye zoezi hilo.

 

Kwa upande wa Mhe. Getama ameishukuru Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kazi nzuri wanayoendelea kuifanya ya kuhakikisha wanatokomeza migogoro ya ardhi katika Mkoa wa Dar es salaam huku.