Habari

NAIBU KATIBU MKUU ARDHI ASISITIZA WELEDI NA MAFANIKIO YA KLINIKI YA ARDHI JIJI LA DAR ES SALAAM

  • 26 Nov, 2024
NAIBU KATIBU MKUU ARDHI ASISITIZA WELEDI NA MAFANIKIO YA KLINIKI YA ARDHI JIJI LA DAR ES SALAAM

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi. Lucy Kabyemera amewataka watumishi wanaoshiriki kuwahudumia wananchi kwenye Kliniki ya Ardhi kufanya kazi kwa juhudi, weledi na ufanisi kwa kuwahudumia wananchi wanaofika kuapa huduma za ardhi.

 

Bi. Kabyemera ameyasema hayo alipokua akizungumza na timu ya Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) iliyoongozwa na Meneja wa Mradi Mijini Bw. Leons Mwenda pamoja na Afisa Maendeleo ya Jamii wa Mradi Bi. Tumaini Setumbi walipotembelea ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.

 

Aidha Naibu Katibu Mkuu Kabyemera amesema kuwa anafahamu kiu ya wananchi wanaohudhuria Kliniki hiyo ni kupata hati pamoja na kutatuliwa changamoto mbalimbali za ardhi ndiyo maana Wizara kupitia Kliniki ya Ardhi imejipanga kuhakikisha inamaliza changamoto zinazohusu ardhi Jijini humo.

 

Zoezi la Kliniki ya Ardhi linaendelea Jijini Dar es salaam eneo la Shule ya Msingi Mzambarauni Kata ya Ukonga na linafanyika kwa wiki mbili ambapo lilianza Novemba 13, 2024 na linatarajiwa kumalizika mnamo Novemba 26, 2024.