Habari

Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wa mwaka 2025 Wapitishwa na Bunge

  • 09 Jun, 2025
Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wa mwaka 2025 Wapitishwa na Bunge

WABUNGE wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameupitisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wa mwaka 2025.

 

Muswada huo wa marekebisho ya sheria umesomwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Deogratius Ndejembi wakati wa kikao cha 42 cha mkutano wa 19 wa Bunge la Bajeti leo Juni 9, 2025 bungeni jijini Dodoma.

 

Muswada huo umefanyiwa marekebisho mbalimbali ikiwemo vifungu vya 12 na 13 vilivyopendekezwa na kurekebishwa kwa lengo la kuondoa wajibu wa mwajiri kukata kodi ya nyumba pamoja na faini ya kuchelewesha kodi.

 

Utaratibu unaopendekezaa waajiriwa watalipa kodi ya pango kama ambavyo wapangaji binafsi wanalipa. Lengo la marekebisho hayo ni kuongeza uwajibikaji wa moja kwa moja kwa mpangaji katika kulipa kodi ili kurahisisha ukusanyaji wa kodi za nyumba za shirika.