Habari

MMUYA AWATAKA WATUMISHI WA ARDHI KUFANYA KAZI KWA KUJITOA NA KUHARAKISHA MIAMALA YA WANANCHI

  • 19 Jun, 2026
MMUYA AWATAKA WATUMISHI WA ARDHI KUFANYA KAZI KWA KUJITOA NA KUHARAKISHA MIAMALA YA WANANCHI

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Kaspar Mmuya, amewataka watumishi wa sekta ya ardhi nchini kufanya kazi kwa kujitoa na weledi ili kutoa huduma bora na za haraka kwa wananchi.

 

Mheshimiwa Mmuya ametoa wito huo leo, Juni 18, 2026, alipotembelea banda la Wizara ya Ardhi kwenye Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali Park, jijini Dodoma.

 

Katika maelezo yake, Naibu Waziri amesisitiza umuhimu wa watumishi kufuatilia kwa ukaribu maendeleo ya miamala ya ardhi kwa kutoa ufafanuzi wa kina pale muamala unapokwama, hatua itakayosaidia kuharakisha mchakato wa upatikanaji wa hati za wananchi.

 

Mhe. Mmuya amesema watumishi wanapaswa kufanya kazi kwa kufuatilia miamala na kutoa ufafanuzi wa kwanini muamala fulani umekwama, ili kuharakisha mchakato wa wananchi kupata hati zao.

 

Aidha, amewataka watumishi hao kuwa tayari kutumia hata muda wao wa ziada nje ya masaa ya kazi ili kushughulikia miamala hiyo, lengo likiwa ni kumaliza changamoto za wananchi kwa wakati na kuongeza ufanisi katika sekta ya ardhi.