Habari

MMUYA ASHIRIKI KIKAO KAZI CHA WENYEVITI WA BODI NA WATENDAJI WAKUU ARUSHA

  • 29 Sep, 2026
MMUYA ASHIRIKI KIKAO KAZI CHA WENYEVITI WA BODI NA WATENDAJI WAKUU ARUSHA

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Kaspar Mmuya, ameshiriki hafla ya ufunguzi wa Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma kinachofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC), jijini Arusha.

 

Hafla ya ufunguzi wa kikao hicho imefanyika leo Septemba 28, 2026, ikiongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi.

 

Kikao hicho kinawakutanisha Wenyeviti wa Bodi, Watendaji Wakuu wa Mashirika ya Umma na wadau mbalimbali kwa ajili ya kujadili namna ya kuimarisha ufanisi, tija na mchango wa taasisi hizo katika maendeleo ya Taifa.

 

Kikao hicho kinafanyika chini ya kaulimbiu isemayo, “Mashirika ya Umma Yenye Ufanisi wa Juu kwa Uchumi Shindani, Shirikishi na Imara katika Kutekeleza Dira 2050.”

 

Kikao hicho cha C-CEOs Forum 2026 kinatarajiwa kuendelea hadi Septemba 30, 2026, na ni jukwaa linaloratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa lengo la kujadili namna ya kuongeza ufanisi wa Mashirika ya Umma na kuhakikisha mipango na shughuli zao zinaendana na vipaumbele vya Dira 2050.